Tetesi za usajili wa Mbwana Samatta Ulaya

0
54

Klabu ya West Brom Albion ya nchini Uingereza inajaribu kuna saini ya mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta ambaye ameripotiwa kuwa anaelekea nchini Uturuki.

Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya England inataka kumnasa nahodha huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 27 ambaye anafanya mazungumzo ya kuhamia Fenerbahce.

Taarifa kutoka Uingereza zinazeleza kuwa West Brom watamchukua Samatta ama kwa mkopo au kumnunua endapo dili litafanikiwa kwani tayari Villa wameonesha kumruhusu kuondoka.

Fenerbahce imekuwa ikimmendea nyota huyo lakini Albion wanaamini kuwa wanaweza kukatisha safari yake ya Uturuki na kumbakisha Uingereza.

Samatta alijiunga Villa Park akitokea Genk ya Ubelgiji Januari mwaka huu baada ya Wesley kupata majeraha. Mkataba wake na Villa unamalizika 2024.

Send this to a friend