TFF yafafanua taarifa ya kufungiwa kwa Waziri Ndumbaro

0
45

Kutokana na mijadala inayoendelea mitandaoni juu ya kufungiwa kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefafanua kuwa Waziri Ndumbaro alishinda rufani ya kesi hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na TFF kwa vyombo vya Habari Septemba 02, 2023 imesema Waziri Dkt. Ndumbaro alifungiwa miaka saba na uongozi uliopita wa TFF na kisha alikata rufani ya kupinga uamuzi huo kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu TFF.

“Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF chini ya uongozi wa sasa ilisikiliza rufani hiyo mwaka 2017 ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro alishinda, hivyo kuondolewa adhabu ya kufungiwa,” imesema taarifa ya TFF.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kwa sasa Dkt. Ndumbaro ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya TFF.

Send this to a friend