TFF ‘yaiba’ tuzo ya Luís Miquissone

0
48

Usiku wa Oktoba 21, 2021 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitoa zaidi ya tuzo 25 kwa kwa wachezaji, kocha na maofisa wengine waliofanya vizuri zaidi katika msimu wa mwaka 2020/21.

Baadhi ya watu wameonesha kutoridhika na namna tuzo hizo zilivyotolewa, hasa tuzo moja ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambayo ilikwenda kwa nyota wa Yanga SC, Feisal Salum (Feitoto).

Baadhi ya waliotoa maoni yao wamesema Feitoto hakustahili kupata tuzo hiyo ikilinganishwa na mmoja wa washindani wake, Luís Miquissone. Kwa mujibu wa takwimu, ni wazi kuwa raia huyo wa Msumbiji alifanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo kuliko Feitoto.

Mshindi wa tuzo hiyo alicheza michezo minne ya ASFC, hakufunga goli kabisa, alihusika katika goli moja (assist).

Kwa uapnde wa Miquissone yeye alishuka dimbani mara tano, akafunga magoli mawili, akatoa usaidizi wa magoli mawili, hivyo kumfanya kuhusika katika magoli manne ya Simba SC.

Kwa takwimu hizo ni wazi kwamba tuzo hiyo ilipaswa kwenda kwa nyote huyo wa Simba ambaye sasa anakipiga katika klabu ya Al Ahly ya nchini Misri. Mbali na hao, mwingine aliyekuwa anawania tuzo hiyo ni John Bocco.

Hata hivyo, ukosolewaji haukuishia hapo, kwani mashabikia hao wa soko wameeleza kuwa Clatous Chama ambaye ameshinda tuzo ya Kiungo Bora, alistahili kuwa Mchezaji Bora, tuzo ambayo imekwenda kwa John Bocco.

Mashabiki hao wamedai kuwa kinachochangia kasoro hizi ni woga wa TFF kuona wachezaji wa timu moja wakishinda tuzo mbalimbali, na kwamba hufanya kuwapa wachezaji wa timu nyingine, ili kuonesha usawa. Hata hivyo, hawajatoa uthibitisho wa madai yao hayo.

Send this to a friend