TFF yaijibu Yanga: Hatuhusiki kualika wageni Mkutano Mkuu wa CAF

0
43

Baada ya viongozi wa Yanga SC kueleza kwamba hawajui kwanini hawakualikwa kwenye mkutano mkuu wa 44 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) licha ya wao kuwa ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.

Yanga yasema TFF ilipaswa kutambua nafasi yao kama mabingwa, mkutano wa CAF

Baada ya shutuma hizo kwamba TFF ilipaswa kutambua nafasi ya Yanga, shirikisho hilo limesema halikuhusika na kualika wageni, bali wote walialikwa na CAF.

TFF imesema jukumu pekee ililofanya ni kutafuta mgeni rasmi mkutano huo ambao umefanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.

Send this to a friend