TFF yamjibu Manara

0
47

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfread amesema amesikitishwa na madai ya aliyekuwa Ofisa wa Klabu ya Yanga, Haji Manara kuwa aliomba msamaha kwa maelezo kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia alifanya makosa.

Kidao amesema maneno hayo si ya kweli, na kwamba Sekretarieti ya TFF haina nafasi ya kuendelea kuzungumzia jambo ambalo tayari limetolewa uamuzi na chombo huru cha TFF.

Manara amefungiwa na Kamati ya TFF kujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili pamoja na faini ya shilingi milioni 20, kwa kosa la kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF.

Send this to a friend