TFF yamzuia Kisinda Yanga

0
57

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiandikia barua Klabu ya Yanga ikiwazui kumleta winga wao nchini, Tuisila Kisinda kwa madai kuwa haiwezi kumtumia kwenye ligi kuu inayorejea Septemba 06, mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti limeripoti kuwa TFF imeizuia Klabu hiyo ikidai tayari Yanga walishakuwa na mchezaji mwingine waliyemwombea uhamisho, licha ya Yanga kudai tayari ilimwondoa mshambuliaji wao Lazarous Kambole kutoka Zambia ili kumsajili Kisinda.

“Wakati tunamsajili Kisinda tulishajipanga tumwondoe nani, na huku kwetu tulishamwondoa Kambole kwa kuwa tuliona hali yake ya majeruhi itatupa shida, tumemwondoa katika mfumo ili nafasi yake ichukuliwe na Kisinda,” imesema Klabu ya Yanga.

Taarifa inasema Klabu hiyo imepanga kutoa malalamiko hayo kwenye kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kupinga uamuzi huo.

Chanzo: Mwanaspoti

Send this to a friend