TFF yatupilia mbali shauri la Fei Toto

0
58

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupilia mbali shauri la mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili.

Kamati hiyo imekutana Machi 02, 2023 kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo la mapitio (review) ya uamuzi wake wa Januari 09, 2023 kati ya Feisal Salum na Klabu ya Yanga baada ya kuwasilishwa na mchezaji huyo dhidi ya klabu yake.

Umri halisi wa wachezaji wote wa Simba na Yanga

“Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili, kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio halina msingi wa kisheria kushawishi kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali, na hivyo imetupilia mbali shauri hilo,” imeeleza taarifa ya TFF.

Aidha, Kamati ya TFF imefafanua kuwa sababu za undani za uamuzi huo zitatolewa siku ya Jumatatu, Machi 06, 2023 kwa pande zote mbili zinazohusika.

Send this to a friend