TFF yaufungia uwanja CCM Liti, Singida

0
89

Kamati ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeufungia uwanja wa Liti, Singida kutumika kwenye michezo ya ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na TFF imesema eneo la kuchezea (pitch) la uwanja huo halifai kuchezewa mpira kutokana na kutokuwa na nyasi kijani kwa sehemu kubwa ya uwanja kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.

“Kufuatia uamuzi huo, timu ya Singida Fountain Gate ambayo inatumia uwanja huo kwa michezo yake ya nyumbani italazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na Kamati ya Leseni za Klabu TFF,” imeeleza.

Send this to a friend