TFF yawafungia Kitumbo na Ulimboka kujihusisha na soka maisha

0
79

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia  maisha wanafamilia wawili kutojishughulisha na mpira wa miguu ambao ni Mwenyekiti wa Kitayosce FC, Yusuph Kitumbo na kocha wa mpira wa miguu, Ulimboka Mwakingwe.

Wawili hao wametiwa hatiani kwa kujihusisha na upangaji wa matokeo katika mechi ya ligi ya Championship kati ya Fountain Gate FC na Kitayosce FC iliyochezwa Aprili 29, mwaka huu mjini Gairo, Morogoro.

Kamati ya TFF imesema Kitumbo hakufika mbele ya kamati bila ya kutoa udhuru wowote wa maandishi ya kupokea wito, wakati Mwakingwe aliwasilisha utetezi wake kwa njia ya maandishi.

Kamati imeeleza kuwa uamuzi kamili utatolewa kwa maandishi kwa pande husika katika mashauri hayo mawili.

Send this to a friend