Thabo Bester na Dkt. Nandipa warejeshwa Afrika Kusini

0
58

Tanzania imerejesha Thabo Bester maarufu ‘Mbakaji wa Facebook’ aliyekamatwa jijini Arusha baada ya kutoroka gerezani nchini Afrika Kusini kwa kudanganya kuhusu kifo chake.

Bester amesafirishwa hadi nchini Afrika Kusini kwa ndege maalum ya kukodi, pamoja na mpenzi wake Dkt. Nandipa Magumana ambaye walikamatwa pamoja huku baba mzazi wa Nandipa, Zolile Sekeleni na mlinzi wa gereza, Senohe Matsoara wakishtakiwa kwa mauaji, kuchoma moto na kusaidia kutoroka kwa Bester.

Kampuni ya Australia iliyofutiwa leseni yatishia kukamata ndege ya Tanzania

Bester amepelekwa katika gereza lenye ulinzi mkali katika Mji mkuu, Pretoria, huku mpenzi wake akifikishwa mahakamani huko Bloemfontein kwa mashtaka ya mauaji, ulaghai na kumsaidia Bester kutoroka.

Bester alikuwa mahabusu kwa mwaka mmoja baada ya kudhaniwa kuwa alifariki kwa kujichoma moto katika chumba chake cha gereza katika mji wa Bloemfontein nchini Afrika Kusini.

Msako mkali ulianzishwa mwezi uliopita baada ya uchunguzi mpya kubaini kuwa mwili huo haukuwa wake.

Send this to a friend