Thamani ya maiamala ya simu kwenye Pato la Taifa yafikia 66%

0
41

Thamani ya miamala ya simu katika pato la Taifa (GDP) imepanda kutoka asilimia 40 kwa mwaka 2013 hadi asilimia 66 kwa mwaka 2021.

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, akifungua mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Huduma Jumuishi za Fedha Kanda ya Afrika kwa njia ya mtandao unaofanyika jijini Arusha kwa siku tatu.

Dkt. Nchemba amesema Tanzania ina mengi ya kuelezea kuhusu teknolojia ya kidigitali katika kuchochea huduma jumuishi za fedha na maendeleo ya uchumi kwa kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2013 na 2017 wananchi waliopata huduma rasmi za fedha walikuwa asilimia 57 na 65 wakati mwaka 2006 wananchi walitumia huduma hiyo rasmi walikuwa asilimia 11.

“Serikali ilitengeneza mazingira wezeshi ya huduma za kifedha na kuruhusu huduma hizo kwa njia za simu za mkononi kwa kushirikiana na benki jambo lililoongeza wigo wa huduma za fedha na kupunguza gharama za miamala,” ameeleza.

Wakili: Wabunge 19 wataendelea kuwa wabunge, kesi haijafutwa

Amesema kuwa watumiaji wa miamala kwa njia ya simu wawamefikia milioni 35.3 hadi Desemba 2021 ikiwa ni asilimia 61 ya jumla ya idadi ya watanzania.

Waziri Nchemba ametumia jukwaa hilo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza Tanzania na kuwaahidi kutoa ushirikiano kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Send this to a friend