Thamani ya mikataba ya matangazo ya mpira katika nchi za Afrika

1
41

Mei 25, 2021, mpira wa miguu nchini Tanzania ilipiga hatua nyingine baada ya Azam Media Limited na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutiliana saini mkataba wa kuonesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka 10.

Mkataba huo uliotiwa saini Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando na Rais wa TFF, Wallace Karia ni wenye thamani ya $100 milioni (TZS bilioni 225.7).

Baada ya kusainiwa mkataba huo kumekuwa na majadiliano kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, wengi wakijiuliza kama ni mkataba wenye tija kwa soka la Tanzania.

Wakati mjadala huo ukiendelea, ni vyema ikafahamika pia baadhi ya mikataba ambayo imeingiwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kurusha matangazo ya mpira wa miguu kwa nchi husika.

Afrika Kusini imeingia mkataba wa miaka mitano (2020-2025) na SuperSport ya nchini humo wenye thamani ya $227 milioni. Nigeria kwa upande wake imeingia mkataba wa miaka 5 na Next TV ya nchini China, mkataba wenye thamani ya $225 milioni.

Morroco ilikuwa na mkataba wa $25.5 milioni na SNRT Group ya Morocco, mkataba uliokuwa wa miaka mitatu (2007-2010). Start Times ya China ilinunua haki ya kurusha matangazo ya soka la Ghana kwa miaka mitano (2020-2025) kwa $5.25, wakati Kenya imeingia mkataba na kampuni hiyo kwa miaka 10 (2021-2031) mkataba wenye thamani ya $1.1 milioni.

Zambia iliingia mkataba wa miaka mitano (2015-2020) na kampuni ya Super Sports ya Afrika Kusini wenye thamani ya $5 milioni.

Kwa mifano hiyo kidogo, inaweza kumpa mwangaza mdau wa mpira wa miguu nchini kunyambua endapo mkataba wa Azam na TFF ni wenye tija katika soka la Tanzania ama la.

Lakini ikumbukwe pia kuwa, mbali na uwekezaji huo uliofanywa na Azam, katika msimu wa 2021/2024, timu zitakazoshiriki ligi kuu zitapata bonasi kama ifuatavyo (TZS);

  1. Milioni 500
  2. Milioni 250
  3. Milioni 225
  4. Milioni 200
  5. Milioni 65
  6. Milioni 60
  7. Milioni 55
  8. Milioni 50
  9. Milioni 45
  10. Milioni 40
  11. Milioni 35
  12. Milioni 30
  13. Milioni 25
  14. Playoff. Milioni 20
Send this to a friend