The Citizen yaamriwa kumlipa Mchechu fidia ya TZS bilioni 2

0
35

Gazeti la The Citizen la nchini Tanzania limeamriwa kumlipa fidia ya TZS bilioni mbili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha habari zilizomshushia hadhi.

Hukumu hiyo imetolewa Machi 03, 2023 na Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam, ambapo imeeleza kuwa gazeti hilo lilichapisha taarifa ambazo zilimtuhumu Mchechu juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kutumia maneno yaliyoshusha hadhi yake.

Gazeti hilo lilidai kunukuu maneno ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli alipokuwa akizindua mradi wa nyumba za NHC zilizopo mkoani Dodoma mwaka 2017.

Jeshi la  Polisi: Tumeona video za askari, tunafanya uchunguzi pamoja na kumpima

Mchechu aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili Desemba, 2017 kisha alirudishwa tena kwenye nafasi hiyo na Rais Samia Suluhu mnamo Machi 14, 2022 kabla kuteuliwa kuwa Msajili wa Hazina Februari 24, mwaka huu.

Send this to a friend