Tiba 5 za asili za magonjwa mbalimbali unazoweza kuandaa nyumbani

0
39

Wazee wa zamani waliamini katika tiba za asili na hadi leo wengi wao bado wanazitumia. Habari njema ni kwamba baadhi ya tiba hizo zimethibitishwa kwa njia za kisayansi kwamba zinafanya kazi ikiwa zitatumiwa vizuri.

Punguza kutumia dawa zenye kemikali na ujaribu kutumia tiba za asili kisha utaona matokeo. Hizi ni baadhi ya tiba hizo;

1. Pilipili- hutibu maumivu
Pilipili ina kiungo ambacho kina umuhimu mkubwa wa tiba tangu jadi na sasa, matumizi yake yameanza kukubalika na wengi sio tu kupitia chakula lakini pia kama dawa.

Ina kiungo kijulikanacho kama capsaicin ambacho kinatumiwa kudhibiti maumivu. Inafanya kazi kwa kuwasha sehemu ya ngozi na kuipa joto.

2. Tangawizi – hutibu maumivu na kichefuchefu
Imebainika kwamba tiba hii ina uwezo mkubwa sana wa kukupa afueni kwa mgonjwa wa mafua au koo kukoroma na kuzuia kichefuchefu pia.

Tangawizi pia ina viungo vya kutuliza maumivu na mara nyingi hata dawa za homa na mafua zimetegenezwa kwa baadhi ya viungo vya tangawizi.

3. Uyoga wa Shiitake- huzuia kansa ya matiti
Lentinan, al maarufu kama AHCC ni kiungo kinachotoka kwenye uyoga wa Shiitake ambacho huzua uvimbe wa seli na husaidia kabisa mchubuko wa uvimbe unaoweza kusbabisha kansa .

4. Lavender (mrujuani) – Kuumwa na kichwa na uchovu
Maumivu ya kichwa wakati mwingine yanaweza kukupata ghafla bila kuwa na dawa za kupunguza makali yake. Iwapo utakumbwa na maumivu haya basi tumia lavender au majani yake itakusaidia pia kupunguza uchovu na matatizo ya kifikra.

5. Vyakula vyenye Magnesium – Hutibu magonjwa mengi
Iwapo kuna kiungo kinachoweza kukupa ahueni ya matatizo mengi nyumbani basi ni vyakula vyote vyenye madini ya magnesium. Iwapo utapatwa na matatizo kama uchovu, kuumwa na kichwa na maumivu ya misuli basi tiba hii ya nyumbani itakupa afueni.

Vyakula vyenye magnesium ni kama Spinachi, parachichi, chokolati nyeusi, maharagwe, mbaazi, ndizi.

Send this to a friend