Tiba rahisi ya kutengeneza nyumbani ya kuondoa weusi kwenye makwapa

0
45

Baadhi ya watu hushindwa kuvaa mavazi yatakayoacha wazi makwapa yao kwa sababu ya rangi nyeusi iliyopo kwenye makwapa. Hili ni tatizo ambalo unaweza kuliondoa unapokuwa nyumbani bila kutumia gharama kubwa.

Juisi ya limao
Matumizi ya juisi ya limao ni moja ya njia zinazoaminika katika kuondoa weusi uliopo kwenye makwapa na kurudisha ngozi yake ya asili. Unachotakiwa kufanya ni kupaka katika maeneo hayo kila siku.

Maziwa
Maziwa yanatajwa kuwa tiba nzuri ya kuondoa weusi kwenye makwapa. Kwa kawaida maziwa yamebeba vitamini vya asili pamoja na asidi ya mafuta ambayo huondoa kwa haraka weusi .

Hii ni namna ya kutengeneza:
Chukua vijiko viwili vya maziwa, kijiko kimoja cha siagi na kijiko kimoja cha unga kisha changanya na upakae katika eneo hilo.

Maganda ya machungwa
Wakati unakula machungwa usiyatupe maganda yake kwa sababu yanaweza kukupa matokeo mazuri kwa wale wenye makwapa yenye rangi nyeusi

Unachotakiwa kufanya ni kuyaanika maganda kwenye jua kwa siku kadhaa, kisha yasage sage maganda hayo kwa kutumia kifaa maalumu cha kusagia mpaka yageuke kuwa unga halafu upakae kwenye makwapa.

Send this to a friend