Tigo na Seedstars zaungana kufanikisha mkutano wa wajasiriamaali wa teknolojia nchini Tanzania
Wajasiriamali wa teknolojia nchini Tanzania wameungana kushiriki katika mkutano wa kimataifa kupitia njia ya mtandao kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo na jinsi ya kuweza kukuza mapato husasani katika masoko machanga. Mkutano huo uliopewa jina la Online Seedstars Summit 2020 ulianza majira ya saa tisa mchana, EAT, kwa nchini Tanzania ulidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Seedstars, kampuni ya kibinafsi ya nchini Uswisi inayojihusisha kwa kiasi kubwa na kugusa maisha ya watu kupitia teknolojia na ujasiriamali hasa katika masoko yanayochipukia.
Wakati wa mkutano huo, wajasiriamali wa ndani walipata fursa ya kujifunza na kugundua mambo yanayofanya vizuri kwa sasa katika ulimwengu wa teknolojia hususani kutoka katika masoko yanayochipukia. Walipata fursa ya kusikia kutoka kwa wagunduzi, viongozi pamoja na waanzilishi kabla ya kumaliza kwa kuangalia fainali za za shindano la dunia la Seedstars ambalo liliwaleta pamoja wajasiriamali zaidi ya 5000 kutoka katika mataifa 83 ulimwenguni.
Mradi wa Ujasiriamali wa Tigo kwa kushirikiana na Seedstars umelenga kutoa mafunzo ya kina kwa watu na makampuni machanga ya kiteknoloiia ili kuyawezesha kupiga hatua na kuweza kupata fedha za kujiendesha kutoka kwa wawekezaji. Miradi hii kwa pamoja inalenga kuinua ujasiriamali kama taaluma inayojitosheleza na hivyo kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapa nyezo nan a elimu itakayowafanya waweze kuendeleza biashara zao. Mkutano huo ukiwa umewezeshwa na Seedstars, kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa wa wajasriamali wa teknolojia katika masoko yanayochipukia, utatoa takwimu, mawazo ya wataalam pamoja na mafundisho mbalimbali kutoka kwa wataalam ili ziweze kuwasaidia washiriki.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo Tanzania, Pavan Ramadhani, amesema, “Kama mshirika wa kiwango cha dhahabu katika madarasa ya Seedstars nchini Tanzania, Tigo inadhamiria kujipambanua kama mwezeshaji mkuu wa makapuni yanayochipukia ya kiteknolojia kwa kutoa fedha pamoja na ushauri wa kitaalam kwa mwaka mzima. Hii itafanikiwa kwa kuwainua vijana wanaojihusisha na teknolojia ili waweze kuonyesha uwezo wao katika kutengeneza mifumo na majawabu kwa changamoto zinazotukumba kwa sasa ikiwa ni pamoja na suala la ukosefu wa ajira kwa vijana.”
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya mkutano kwa niia ya mtandao, Mkurugenzi Mtendaji wa Koncept Advertising Agency, kampuni inayojihusisha na masuala ya matangazo kupitia mtandao, Krantz Mwantepele, amesema,”Kama mjasiriamali, naamini hizi fursa muhimu sana kwani zitatoa mwongozo juu ya namna tunavyopaswa kufanya shughuli zetu na jinsi tunavyoweza kuitumia teknolojia katika kukuza vyanzo vyetu vya mapato.”
Mkutano huu wa kwanza ambao Tigo Tanzania wameudhamini, umewaleta pamoja washiriki zaidi ya 5000 kutoka katika mataifa 83 duniani. Tigo Tanzania inatarajiwa kushriki kikamilifu katika shughuli zote za Seedstars nchini Tanzania kwa mwaka mzima.