Tiktok yasababisha kwenda jela miaka mitatu

0
2

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa TikTok nchini Indonesia amehukumiwa kifungo cha karibu miaka mitatu jela baada ya kuripotiwa kuzungumza na picha ya Yesu kwenye simu yake na kumwambia akate nywele.

Ratu Thalisa aliyebadili jinsia, alikuwa mubashara kwenye ukurasa wake wakati akijibu maoni ambayo yalimwambia akate nywele zake ili aonekane zaidi kama mwanaume.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja mara baada ya makundi mengi ya Kikristo kuwasilisha malalamishi kwa polisi dhidi ya Bi Thalisa kwa kukufuru.

Mahakama imesema maoni yake yanaweza kuvuruga maelewano ya kidini katika jamii, na ikamshtaki kwa kukufuru.

Hukumu hiyo imepingwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu likiwemo shirika la Amnesty International ambalo limeeleza kuwa ukiukaji wa uhuru wa kujieleza wa Ratu Thalisa na kutaka ifutiliwe mbali.

Send this to a friend