Timu itakayoshindwa kufika uwanjani kupokonywa alama 15
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema timu itakayokosa kufika uwanjani na kusababisha mchezo kutofanyika baada ya kushiriki kikao cha maandalizi ya michezo, itatozwa faini ya TZS milioni 5.
Hayo yamesemwa katika kanuni mpya ya 31 iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu leo Agosti 15, 2022 ambayo imeeleza kuwa, mbali na kutozwa faini hiyo, timu italazimika kulipa fidia ya uharibifu wowote unaoweza kujitokeza pamoja na kupokonywa alama 15.
Bodi ya Ligi yaruhusu wachezaji 12 wa kigeni kwenye mchezo mmoja
Kanuni hiyo inaeleza kuwa kwa viongozi watakaosababisha jambo hilo watachukuliwa hatua zaidi za kinidhamu.