Timu za Sudan Kusini zakosa viwanja vya nyumbani

0
105

Timu zilizoingia klabu bingwa barani Afrika kutoka nchini Sudan Kusini zimekosa uwanja wa kuchezea nyumbani kutokana na viwanja vyao kukosa vigezo vilivyoidhinishwa na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF).

Katika mkutano wa 44 wa CAF uliofanyika  leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na wanachama mbalimbali wa Shirikisho wakiongozwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe, imetolewa orodha ya timu na viwanja vyao vitakavyotumika katika mashindano hayo.

Waziri Mkuu amwalika Rais wa CAF mechi ya Simba na Yanga

Kutokana na hatua hiyo, timu hizo zitalazimika kucheza kwenye viwanja vya nchi nyingine katika michezo yao ya nyumbani, uwezekano mkubwa ukiwa kutumia viwanja vya nyumbani vya timu pinzani.

Moja ya timu kutoka nchini Sudan Kusini, Zalan FC imepangwa kucheza na Young Africa (Yanga)  kutoka Tanzania katika hatua ya awali ya mashindano ya klabu bingwa.