Timu za Taifa zatengewa milioni 183

0
42

Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kiasi cha shilingi milioni 183.5 kimetengwa katika mwaka huu wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kuhudumia timu za Taifa.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma leo Septemba 22, 2022 wakati akijibu swali la Janeth Elius Mahawanga ( Viti Maalum) aliyeuliza ni lini Serikali itawekeza katika sekta ya michezo hasa kwenye timu za wanawake, ili kuibua vipaji kwa watoto.

“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika timu za Taifa za wanawake ambapo kupitia uwekezaji huu, timu hizi zimeendelea kufanya vizuri katika ukanda wa CECAFA na COSAFA na pia umeiwezesha timu ya Serengeti Girls kufuzu mashindano ya kombe la dunia nchini India,” amesisitiza Naibu Waziri Gekul

Aidha, Naibu Waziri ametumia nafasi hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha michezo hiyo ambayo inaendelea kuzalisha wanamichezo wengi nchini.

Send this to a friend