TMA: Kimbunga ‘Freddy’ hakina madhara ya moja kwa moja

0
43

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kwa takribani wiki sasa mamlaka imekuwa ikifuatilia mwenendo wa kimbunga “Freddy” kilichopo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi karibu na Pwani ya Madagascar na kujiridhisha kutokuwa na madhara ya moja kwa moja kwa sasa kwa maeneno yaliopo nchini.

Taarifa hiyo imetolewa Februari 20, 2023 ili kutoa ufafanuzi juu ya taharuki iliyozuka katika mitandao mbalimbali kuhusu uwepo wa kimbunga hicho ambapo mamlaka imesema ni kosa kisheria kwa mtu mwingine kutoa taarifa za tahadhari kwani ndiyo imepewa jukumu kisheria kufuatilia na kutoa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa jamii.

Jeshi la Polisi lasema halina utani

“Mamlaka inapenda kuikumbusha jamii na umma kwa ujumla kuwa kwa mujibu wa sheria ya Mamkala ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya 2019, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutoa taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa, na ni kosa kisheria mtu mwingine kufanya hivyo,” imesisitiza TMA.

Aidha, TMA imewashauri wananchi kuendelea kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka sambamba na kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.

Send this to a friend