TMA yatangaza uwepo wa kimbunga IALY

0
20

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga ‘IALY’ katika Bahari ya Hindi Kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

TMA imesema mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo la kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

“Kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katikati kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi,” imeeleza taarifa ya TMA.

Aidha, TMA imesema inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini na kwamba itatoa taarifa kila inapobidi.

Send this to a friend