TMB: Marufuku kutumia magogo buchani

0
49

Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) imewataka wafanyabiashara na wamiliki wa maduka ya nyama kutumia vifaa maalum vya kukata nyama na kuachana na matumizi magogo ya miti ili kulinda afya za walaji.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi, Ofisa mifugo bodi ya nyama Dkt. Mpoki Alilanuswe amesema tayari miongozo na maelekezo vimekwisha tolewa na kilichofuata ni utekelezaji.

“Sekta ya nyama ni sekta nyeti ambayo inahitaji umakini mkubwa kuanzia hatua ya uandaaji kutoka kwenye machinjio mpaka sokoni sasa tunapotoa maelekezo lengo ni kuwepo kwa ubora wa kitoweo hicho kwa walaji,”amesema.

Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe

Dkt. Alinanuswe amesema katika kukabiliana na hali hiyo bado wanaendela kuhamasishaji matumizi ya vifaa vya kisasa kuandaa nyama, ikiwepo magogo ya plastiki wakati wa kukata kitoweo hicho kabla ya bodi kuanza kuchukua hatua za kufanya ukaguzi.

Send this to a friend