Tony Blair aeleza anavyovutiwa na uongozi wa Rais Samia

0
19

Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair amesema Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) inaunga mkono jitahada mbalimbali zinazochukuliwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Kiongozi huyo amesema hayo alipofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kufanya mazungumzo na Rais Samia.

Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Send this to a friend