Tozo: Serikali kutoa milioni 500 kila jimbo

0
66

Serikali imesema inakusudia kutoa shilingi milioni 500 kila jimbo nchini kwa ajili ya kukarabati barabara za vijijini ikiwa ni sehemu ya matumizi ya fedha zinazokusanywa kupitia tozo za miamala ya simu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Ddodoma kuhusu punguzo la asilimia 30 ambalo serikali imelifanya kwenye tozo hilo.

“Hii Septemba iliyoanza mpaka inavyoisha kutakuwepo na takribani milioni 500 kila jimbo kwa ajili ya kwenda kutengeneza zile barabara za vijijini,” amesema Nchemba.

Aidha, amesema fedha zinazokusanywe kwenye miamala pia zitatumika kwenye sekta za kijamii kama afya, maji na elimu ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ambazo zimekuwa zikiwakumba.

Kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 63 ambazo zimekusanywa hadi Agosti 30 mwaka huu, Waziri Nchemba amesema sehemu ya fedha hizo itatumika kumaliza changamoto ya sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa ambazo hazikuwahi kuwa na vitu tangu uhuru.

Ametumia mkutano huo kukanusha taarifa kuwa tozo zimesababisha miamala ya simu kupungu na kueleza kwamba, “kabla ya kuanza kwa tozo kulikuwa na miamala milioni 10 hadi milioni 11 lakini sasa kuna miamala milioni 10, milioni 9.8, milioni 9.9.”

Mengine aliyogusia kwenye mkutano huo ni;

Send this to a friend