Tozo ya ving’amuzi yashuka

0
45

Serikali imepunguza kiwango cha tozo za ving’amuzi kwa kiwango cha shilingi 500 hadi shilingi 2000, itakayokuwa ikitozwa kupitia malipo ya vifurushi.

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Sillo Baran wakati akiwasilisha maoni ya kamati ya bajeti, katika mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha Mwaka 2022.

Kabla ya punguzo hilo, Serikali ilitoa pendekezo la kuanzisha tozo ya shillingi 1000 hadi shilingi 3000 kwa ving’amuzi.

Tanzania mwenyeji tuzo za MTV Africa Music Award 2023

Hata hivyo, baada ya majadiliano hayo ya kina ilionekana kwamba kiwango hicho ni kikubwa, hivyo kamati ilipendekeza kuanza kutoza kati ya shilingi 500 hadi Shilingi 2000.

Tayari bunge limepitisha muswada wa huo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ushauri wa wabunge umezingatiwa katika kuhakikisha maslahi ya nchi yanapatikana.