Tozo za miamala ya simu zapunguzwa kwa 40%

0
40

Serikali ya Tanzania imepunguza tozo za miamala ya kieleketroniki (simu) kwa asilimia 30, Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza.

Aidha, serikali imefanya mazungumzo na kampuni za simu ambazo zimeridhia kupunguza viwango vya tozo kwenye miamala ya kutuma na kutoa fedha katika mtandao na mtandao mwingine kwa asilimia 10.

Hayo yameelezwa na wizara hiyo kufuatia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kutia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za kutuma na kutoa fedha za mwaka 2021.

Aidha, wizara imesema kuwa viwango vilivvyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la serikali kesho Septemba 1, 2021.

Hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko ya wananchi waliokuwa wakieleza kwamba tozo hizo zilikuwa juu sana, na kuitaka serikali kuzifanyia marekebisho.

Send this to a friend