TPA: Hakuna mgomo wala hujuma Bandari ya Dar es Salaam

0
12

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema hakuna mgomo wala hujuma zozote katika Bandari ya Dar es Salaam na badala yake kazi za uhudumiaji meli na shehena zinaendelea kutekelezwa katika magati yote.

Kauli hiyo imekuja baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii taarifa za kudorora kwa utendaji kazi ya kuhudumia meli na shehena katika bandari hiyo kunakohusishwa na mgomo wa wafanyakazi wenye madai mbalimbali ikiwemo kufutiwa mikataba yao ya kazi.

Bunge la Ghana lakatiwa umeme kwa kutolipa deni

“Hakuna mtumishi yeyote wa TPA, (mtumishi wa ajira ya kudumu au mtumishi wa ajira za muda maalum) aliyesitishiwa mkataba wake kwa sababu zozote zile. Watumishi wote wanatimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia ratiba za sehemu zao za kazi,” imesema taarifa iliyotolewa na TPA.

Aidha, TPA imesema imejipanga kuanza kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaobainika kuhusika na upotoshaji huo ambao umezua taharuki kwa jamii.

Send this to a friend