TPSF: Adhabu za kufungia maeneo ya biashara itolewe na mahakama

0
41

Kufuatia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kufungia jumla ya baa na kumbi za starehe 89 baada ya kusababisha kelele zinazozidi viwango vilivyopendekezwa, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeshauri kuwa mahakama pekee inatakiwa kutumika katika utoaji wa adhabu ya kufungia maeneo hayo.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa TPSF, Raphael Maganga ameshauri sheria inayohusika katika utoaji wa adhabu hizo itazamwe upya, utoaji wa vibali vya biashara hizo baada ya kujihakikishia mazingira yatakayotumika kwa biashara hizo pamoja na kuendelea na utoaji wa elimu katika makundi ya wafanyabiashara.

Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe

“Kuna wengine wanapewa leseni za biashara wanawekeza hadi TZS bilioni 20 lakini baadaye anafuatwa kwa vigezo hivyo na kufungiwa, sasa kabla ya leseni waende kukagua. Wakati mwingine unakuta leseni eneo moja watu kumi, hilo ni changamoto na litazamwe,” amesema.

Aidha, amesema tukio la kufungiwa maeneo hayo lilitengeneza mshtuko pamoja na kusababisha athari kubwa za kiuchumi huku likienda kinyume na malengo ya Serikali inayopambania kuweka mazingira bora ya biashara kupitia hatua za kupunguza vikwazo ili wafanyabiashara kufanya kazi kwa amani zaidi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend