TRA: Kodi ya matangazo ya Facebook haiwahusu wanaotumia akaunti binafsi

0
21

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa utozaji wa kodi kwa watoa huduma za kielektroniki unawahusu wafanyabiashara wasio wakaazi wanaofanya biashara kwa njia ya mtandao ambao awali walikuwa hawalipi kodi.

TRA imeeleza hayo siku chache baada ya kampuni ya Meta kueleza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu itaanza kutoza kodi ya asilimia 18 ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye matangazo yanayowekwa kwenye mtandao huo.

“Ifahamike wazi kuwa kodi hii haiwahusu wateja binafsi wanaotumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram kutangaza biashara zao,” imeeleza TRA ikisisitiza kuwa “inawahusu wafanyabiashara ambao wana mikataba ya kibiashara na mitandao hiyo ya kijamii.”

Nchi 10 za Afrika zenye miundombinu bora ya barabara

Mamlaka hiyo imesema ilifanya mabadili ya sheria ili kuwajumuisha wafanyabiashara hao ambao awali walikuwa hawalipi kodi tofauti na wafanyabiashara wa kawaida (wale walio na makazi Tanzania) wanaotoa huduma zinazofanana na hizo.

Send this to a friend