TRA kutaifisha magari yenye namba zisizotambulika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa onyo kwa watumiaji wa namba za usajili wa magari ambazo hazitambuliki na TRA au taasisi nyingine za Serikali zilizopewa jukumu hilo kisheria.
Aidha Mamlaka imetoa onyo kwa wamiliki wa magari kutumia vibati vya namba vyenye rangi zisizotambulika kisheria vinavyowekwa mbele na nyuma ya vyombo vya moto (number plate).
Dawa bandia za nguvu za kiume zakamatwa Geita
Hivyo, wamiliki wa vyombo vya moto na umma kwa ujumla wametangaziwa kuwa utengenezaji na matumizi ya vibati hivyo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973.
TRA imetangaza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka sheria hii ikiwa ni pamoja na kutaifisha chombo cha moto husika.