TRA yavunja rekodi, yakusanya trilioni 3.05 Desemba

0
26

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 (Julai hadi Desemba) imefanikiwa kukusanya kiasi cha TZS trilioni 13.92 ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.98 ya lengo la kukusanya TZS trilioni 14.21.

Makusanyo hayo ya nusu mwaka ni ongezeko la asilimia 11.5 ukilinganisha na makusanyo ya TZS trilioni 12.49 yaliyofikiwa katika kipindi kama hicho, katika mwaka wa Fedha uliopita 2022/2023.

Aidha, katika kipindi cha Desemba 2023 TRA imekusanya TZS trilioni 3.05 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 102.99 ya lengo la kukusanya kiasi cha TZS trilioni 2.96.

“TRA imefanikiwa kuandika rekodi mpya ya kiwango cha juu cha makusanyo kwa mwezi tangu kuanzishwa kwake,” imesema taarifa ya TRA.

Imeongeza kuwa makusanyo hayo ni ongezeko la asilimia 9.02 ukilinganisha na kiasi cha TZS trilioni 2.79 kilichokusanywa katika mwezi kama huo katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Send this to a friend