TRC yafanya mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za SGR

0
86

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za treni za reli ya kiwango cha mataifa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro kuanzia Julai 05 mwaka huu.

TRC imesema ongezeko la safari litahusisha kuanza kwa treni mpya ya haraka (express train) ambayo itakuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Morogoro bila kusimama vituo vya kati.

“Mabadiliko ya ratiba yatakuwa kama ifuatayo; Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku. Treni itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 1:30 usiku.

Imeeleza kuwa treni ya kawaida itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa 10:00 jioni huku Morogoro ikiondoka saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.

Aidha, abiria wameshauriwa kukata tiketi kupitia njia ya mtandao au madirisha ya tiketi yaliyo ndani ya vituo vya treni saa 2 kabla ya muda wa safari kuepuka msongamano, huku TRC ikieleza kuwa itaendelea kuongeza idadi ya safari kulingana na ongezeko la abiria ili kutoa huduma bora.

Send this to a friend