TRC yaomba radhi kwa treni kuchelewa kutokana na hitilafu

0
88

Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeomba radhi kwa abiria waliosafiri kutoka Dodoma saa 2: 15 usiku kuelekea Dar es Salaam Agosti 01, 2024 kwa treni ya mwendo kasi kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema hitilafu za kiufundi zilitokea eneo la Mtaa wa Mshikamano Kata ya Kihonda mkoani Morogoro majira ya saa 4:33 na kushughulikiwa kwa muda wa takriban saa moja, na kusababisha treni hiyo kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar es Salaam kwa wakati uliopangwa.

“Shirika la Reli Tanzania linatoa taarifa kuwa treni ya abiria iliyobeba viongozi na wananchi wengine walioko Dodoma saa 1 usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yoyote,” imesema TRC.

Aidha, TRC imesema inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha madhara kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa reli na linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Send this to a friend