TRC yaomba radhi treni ya umeme kuzima kwa saa mbili

0
38

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika ya stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha Kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili Julai 30, 2024.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk imesema taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama aina ya ngedere au bundi wanapogusa nyasa zilizotandazwa juu ya reli.

“Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku,” imeeleza taarifa yake.

Aidha TRC imesema mafundi walifanikiwa kuutatua changamoto na kurejesha umeme saa sita na nusu usiku na treni iliendelea na safari kuelekea Dodoma ambapo iliwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.