TRC yasitisha huduma ya usafiri wa treni

0
57

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusitisha huduma ya usafiri wa treni ya abiria inayotoka Dar es Salamam kuelekea mikoa ya Morogoro, Dodoma,  Tabora,  Mwanza, Mpanda na Kigoma kuanzia Machi 28, 2023.

TRC imefafanua kuwa imesitisha utoaji wa huduma hiyo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini na kupelekea daraja kusombwa na maji kati ya stesheni ya Godegode na Gulwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Aidha, imesema huduma inatarajia kurejea siku ya Machi 30, mwaka huu na kwamba shirika linaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma zinarejea kwa haraka.

Send this to a friend