Treni za umeme kuendeshwa kwa umeme wa TANESCO

0
99

Treni ya umeme inayotarajiwa kuanza safari zake Januari 2023 kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR) itategemea umeme unaotolewa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande ambapo amefafanua kuwa SGR inahitaji upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa kudumu.

“Kwa kuzingatia mambo yote hayo, TANESCO ndiyo wasambazaji sahihi wa umeme kwa treni zinazotumia umeme,” amethibitisha Chande.

Rais Samia atengua uamuzi wa TRA kuhusu machinga kutumia EFD

Mwaka 2021 aliyekuwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alisema mradi huo utakapokamilika, treni zinazotumia umeme zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme unaoweza kudumu hadi saa 2, hivyo ikitokea kukatika kwa umeme hata dakika 10 bado treni itaendelea kukimbia.

Tanzania kwa sasa inakabiliwa na mgao wa umeme katika baadhi ya maeneo ya nchi, huku TANESCO ikitoa hakikisho kuwa mgawo huo utaisha mwaka 2025.

Send this to a friend