
Rais Donald Trump amemshutumu Rais wa China, Xi Jinping, Rais wa Urusi, Vladimir Putin pamoja na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kwa kula njama dhidi ya Marekani wakati walipohudhuria sherehe ya kijeshi mjini Beijing.
Maoni ya Trump yamekuja wakati China ikiwa mwenyeji wa viongozi wa ulimwengu katika gwaride kubwa zaidi la Siku ya Ushindi huko Beijing.
Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump aliandika: ” Rais Xi na watu wema wa China wawe na siku nzuri na ya kudumu ya sherehe. Tafadhali fikisha salamu zangu za dhati kwa Vladimir Putin na Kim Jong Un unapopanga njama dhidi ya Marekani.”
Urusi kupitia Msemaji wa Ikulu, Dmitry Peskov imesema hakuna njama yoyote iliyokuwa ikipangwa, na kwamba hata viongozi hao hawakuwahi kufikiria jambo hilo.
Ameongeza kuwa anatumaini kauli ya Trump ilikuwa ya utani akisisitiza kuwa ushirikiano wa Urusi na washirika wake wa Mashariki kama China na Korea Kaskazini unafanywa kwa manufaa ya wote, si dhidi ya taifa lolote.







