Trump akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono

0
44

Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa mwandishi wa jarida, E. Jean Carroll katika duka moja mjini New York miaka ya 1990.

Jopo la majaji tisa lilifikia uamuzi huo baada mashauriano ya chini ya saa tatu siku ya Jumanne ambapo pia imemkuta na hatia ya kumkashifu mwandishi huyo kwa kuita madai yake ni ya uongo.

Mahakama iligundua kuwa Carroll (79) alikuwa amethibitisha vya kutosha kwa mahakama kwamba Trump alimnyanyasa kingono karibu miaka 30 iliyopita katika chumba cha kubadilishia nguo.

Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe

“Leo, ulimwengu hatimaye unajua ukweli. Ushindi huu sio kwangu tu bali kwa kila mwanamke ambaye ameteseka kwa sababu hakuaminiwa,” amesema Carroll katika taarifa iliyoandikwa kufuatia uamuzi huo.

Hata hivyo mahakama haikumkuta na hatia ya kumbaka Carroll kama alivyodai kwa muda mrefu, hivyo imemuamuru kumlipa takribani dola milioni tano [TZS bilioni 11.8] kama fidia.

Ni mara ya kwanza kwa Trump kupatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kingono.

Send this to a friend