
Rais wa Marekani, Donald Trump ametimiza siku 100 Jumanne, tangu aingie madarakani.
Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), imesema tangu kuingia kwake madarakani, imefanikiwa kuokoa takriban dola bilioni 160 [TZS trilioni 430.9] kupitia upunguzaji wa matumizi yasiyo ya lazima, udanganyifu, na matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kupunguza matumizi kadhaa makubwa ambayo yamekuwa yakijadiliwa sana katika miezi ya hivi karibuni.
Moja ya maeneo yaliyolengwa sana na Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) katika muhula wa kwanza wa Rais Trump ni matumizi katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).