Trump asitisha misaada ya kijeshi kwa Ukraine

0
3

Rais wa Marekani, Donald Trump amesitisha misaada yote ya kijeshi kwa Ukraine kufuatia kutokuelewana kwake na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky wiki iliyopita alipowasili ikulu ya Marekani.

Uamuzi huo unaathiri uwasilishaji wa risasi, magari, na vifaa vingine vya kijeshi ikijumuisha shehena iliyokubaliwa wakati Joe Biden alipokuwa Rais.

Ikulu ya White House haijaeleza ni kwa muda gani Marekani itasitisha misaada hiyo kwa Ukraine.

“Rais amekuwa wazi kwamba anazingatia amani. Tunahitaji washirika wetu kujitolea kwa lengo hilo pia,” Afisa wa White House ameeleza na kuongeza kuwa “Tunasitisha na kukagua misaada yetu ili kuhakikisha kuwa inachangia suluhisho.”

Hatua hiyo imekuja baada ya Trump kuilaumu Ukraine kusababisha vita na Urusi huku akimtaja Rais Zelensky kama dikteta huku akisema Zelensky anacheza kamari na vita vya tatu vya dunia.

 

Send this to a friend