
Rais wa Marekani, Donald Trump amesaini agizo la kusitisha ufadhili wa Voice of America (VOA), shirika la habari ambalo linapata fedha kutoka kwa serikali ya Marekani akisema kuwa VOA inampinga Trump na kuwa na misimamo mikali.
Mkurugenzi wa VOA, Michael Abramowitz amesema zaidi ya wafanyakazi 1,300 wa shirika hilo wamepewa likizo ya lazima jambo ambalo limelemaza shirika hilo la utangazaji linalotoa matangazo kwa takriban lugha 50.
Taarifa ya Ikulu ya White House imesema agizo hilo linakwenda kuhakikisha walipakodi wa Marekani hawashiriki tena katika propaganda.
Trump ameagiza utawala wake kupunguza mashirika kadhaa hadi kiwango cha chini kinachohitajika kisheria chini ya agizo lililopewa jina “Kuendelea Kupunguza Urasimu wa Shirikisho.”