Trump atangaza Afrika Kusini haitoalikwa kwenye mkutano wa G20

0
64

Rais Donald Trump amesema Afrika Kusini haitaalikwa kwenye mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika Marekani mwaka ujao, akidai imekuwa ikitekeleza mauaji kwa wazungu (Afrikaans).

Pia, Trump amedai Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alikataa kukabidhi uenyekiti wa umoja huo kwa kaimu balozi wa Marekani ambaye alihudhuria hafla ya kufunga mkutano huo uliofanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Kupitia mtandao wa X, Trump ameandika “Afrika Kusini imeonesha kwa Dunia kwamba si nchi inayostahili uanachama mahali popote, na tunakwenda kusitisha malipo na ruzuku zote kwao, kuanzia sasa hivi.”

Hata hivyo, maafisa wa Afrika Kusini wamesema kuwa makabidhiano hayo yalipaswa kufanywa kwa mkuu mwingine wa nchi, si kwa mwanadiplomasia.

Send this to a friend