Trump atishia kuiongezea China ushuru mwingine wa asilimia 50

0
10

Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuiwekea China ushuru wa ziada wa asilimia 50 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani ikiwa haitafuta ushuru wake wa kulipiza kisasi wa asilimia 34.

China ilijibu vikali Jumapili baada ya Trump kutangaza ushuru huo mpya kwa bidhaa zake. Hata hivyo, Trump ameipa Beijing muda wa saa 24 kufuta ushuru wake, la sivyo bidhaa za China zitakabiliwa na ongezeko hilo la ushuru.

Katika hatua yake ya kujibu, China imesisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa na kwamba itapambana hadi mwisho dhidi ya nyongeza mpya ya ushuru kutoka Marekani.

Ushuru huo mpya unaweza kuacha baadhi ya makampuni ya Marekani yanayoleta bidhaa fulani kutoka China yakikabiliwa na ushuru wa asilimia 104.

Send this to a friend