Trump atishia kuzuia kufunguliwa daraja linalounganisha Canada na Marekani

0
24

Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuzuia kufunguliwa kwa daraja jipya lililojengwa na Canada linalounganisha Canada na Marekani kupitia Mto Detroit, akitaka Canada ikabidhi angalau nusu ya umiliki wa daraja hilo kwa Marekani pamoja na kutimiza masharti mengine ambayo hayajabainishwa.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa Truth Social, Trump amesema hataruhusu kufunguliwa kwa Daraja hilo la Gordie Howe, lenye urefu wa maili 1.5 linalounganisha Detroit na Windsor, Ontario.

 “Sitakubali daraja hili lifunguliwe hadi Marekani ilipwe kikamilifu kwa kila kitu tulichowapa na, muhimu zaidi, hadi Canada iitendee Marekani kwa haki na heshima tunazostahili,” amesema.

Ujenzi wa daraja hilo tayari umekamilika, na linatarajiwa kufunguliwa mwaka huu baada ya kukamilika kwa kipindi cha majaribio.

Send this to a friend