Tshala Muana akamatwa kwa “kumkejeli” Rais kwa wimbo

0
58

Jeshi la polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) linashikilia mwanamuziki Tshala Mauna ambaye alikamatwa Novemba 16, 2020 kwa tuhuma za kumkashifu Rais Felix Tshisekedi.

Mauna mwenye miaka 62 anatuhumiwa kutenda kosa hilo kupitia wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘ingratitude.’

Hata hivyo wimbo huo haujataja jina la kiongozi huyo lakini tafsiri yake unamzungumzia mtu aliyepewa kila kitu maishani lakini ameshindwa kutenda haki na mambo mazuri licha ya kuwa yupo madrakani.

Mauna mwenye uhusiano wa karibu na familia ya Rais Mstaafu wa DRC, Joseph Kabila anashikiliwa kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi kuhusu wimbo wake.

Mbali na kukamatwa kwake, imeripotiwa kuwa wimbo huo umefungiwa.

Maandamano yameripotiwa mjini Kinshasa kufuatia kukatwa kwa nguli hiyo wa muziki.

Send this to a friend