TTB: Hatujamtuma Mwijaku kutangaza utalii Ujerumani

0
95

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema haijamtumia wala kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony maarufu kama Mwijaku nchini Ufaransa kutangaza utalii mitaani, akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na TTB, imesema mwaka huu TTB ilishirikiana na Sekta Binafsi kwenye maonyesho ya utalii ya Ufaransa ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023 na ilikwenda na kampuni 12 ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK ambayo ndiyo ilimgharamia Mwijaku kwenda kufanya utangazaji wa kampuni yake inayofanya biashara ya utalii yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani.

Uwanja wa Mkapa kukamilika ndani ya siku tano

“TTB inakanusha kumtumia Mwijaku na inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania na taratibu zilizowekwa.” imesema taarifa.

Aidha, Bodi ya Utalii imewataka watu wote kuzingatia sheria kwenye utoaji wa taarifa au utangazaji na uhamasisha wa utalii ndani na nje ya nchi.

Send this to a friend