Tulia: Mdee na wenzake wapo bungeni kihalali

0
43

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wabunge 19 wa Viti Maalum wa CHADEMA wapo bungeni kihalali.

Dkt. Tulia ambaye ameanza kutumilia wadhifa huo Februari Mosi mwaka huu amesema hayo wakati akijibu swali la Mwandishi wa Mwananchi Communication Limited, Nuhu Shija aliyetaka kujua uhalali au uharamu wa wabunge hao bungeni.

Spika amesema kwa uwepo wao bungeni, basi wapo kihalali kwani hakuna mtu ambaye hajakidhi vigezo aliyepo bungeni, ambapo sharti mojawapo ni udhamini wa chama cha siasa.

Aidha, kuhusu mchakato wa wabunge hao kufika bungeni, amesema bunge halihusiki na mchakato huo, kwani wao wanahusika na majina yaliyoletwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ndio walioapishwa.

Ameeleza zaidi wabunge wamekuwa wakiondolewa bungeni wanapovuliwa uanachama wa vyama vyao, na kwamba wakipata taarifa na nyaraka halali kutoka kwenye chama chochote kuhusu kuwavua uanachama wabunge au mbunge, basi uhalali wao utakoma.

Kuhusi bunge kuwa na wwabunge wengi zaidi wa CCM, Dkt. Tulia amesema hilo si tatizo kwani wananchi ndio wanaoamua wamtume nani awawakilishe bungeni.

Send this to a friend