Tulia: Ofisi ya Spika haina taarifa za Wabunge waliofukuzwa CHADEMA

0
35

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa ofisi ya Spika wa Bunge haina taarifa za wabunge wa viti maalum kufukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Dkt. Tulia amesema hilo bungeni Dodoma leo wakati wa mjadala bungeni baada ya Mbunge Jesca Kishoa katika maelezo yake kusema kuwa amefukuzwa uanachama wa chama hicho.

“… Nikiwa kama Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA kabla sijaondolewa kwenye chama changu [CHADEMA]…,” amesema Kishoa.

Hata hivyo Naibu Spika alimtaka kufuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa wabunge wote waliomo bungeni wana vyama vya siasa na kwamba angekuwa amefukuzwa, basi asingekuwemo bungeni.

Sikiliza maelezo hayo hapa chini;

Send this to a friend