Tume ya Rais yakutana na Majaliwa

0
25

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imekutana na Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa leo katika ukumbi uliopo Jengo la Takwimu mkoani Dodoma.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pamoja na kujadili namna ya kuondokana na matukio hayo.

Tume hiyo inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa matukio hayo na kukusanya taarifa ambazo zitawasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria ili kudhibiti vitendo hivyo visije kutokea tena.

Send this to a friend